Search This Blog

Monday, August 3, 2020

Akaunti Ya ‘NBC Shambani’ Yawavutia Wadau Maonesho YaNanenane Simiyu

Wadau mbalimbali wa kilimo wanaoshiriki na kutembelea Maonyesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, wameonesha kuvutiwa na huduma mpya ya NBC Shambani ambayo imebuniwa mahususi kuenda sambamba na mahitaji ya huduma za kifedha ya wadau hao.

Akifafanua kuhusu huduma hiyo mpya kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda la benki hiyo kwenye maonesho hayo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati, kutoka benki hiyo Bw Raymond Urassa alisema inalenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

“Lengo hasa la huduma hii ya NBC Shambani ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.

Mbali na kuwawezesha wakulima hao kutunza fedha zao kwa urahisi, Bw UIrassa alizitaja baadhi ya faida za huduma hiyo kwa mkulima mmoja mmoja kuwa ni pamoja na mkulima kupata faida kwa salio la akiba linalozidi sh 100,000 na kuendelea huku pia kukiwa hakuna makato ya kila mwezi.

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.

Wakizungumzia huduma hiyo, baadhi ya wadau wa kilimo walisema imekuja wakati muafaka kwa kuwa kwasasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo ambayo ustawi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinaenda sambamba na mahitaji wa wadau hao.

“Nimeona kupitia huduma hii mkulima anaweza kuweka na kutoa kiasi chochote cha fedha tena kwa wakati wowote. Huo ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimo tunahitaji ili kufanikisha miamala yetu wakati wowote hususani tunapofanya manunuzi ya pembejeo za kilimo au kuhifadhi fedha baada ya kufanya biashara,’’ alisema Bw Emmanuel Rutatora ambae ni mkulima kutoka wilaya ya Rorya.
 Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati, kutoka benki hiyo Bw Raymond Urassa (Kulia) akiwakaribisha baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo walipotembelea banda  la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maonyesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Pamoja na mambo mengine wadau hao walionyesha kuvutiwa zaidi na akaunti  ya benki hiyo inayofahamika kama "NBC Shambani' ambayo imebuniwa mahususi kwenda sambamba na mahitaji ya huduma za kifedha ya wadau hao. 
Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NBC Bw Peres Mbogoma (Kulia) akiwaonyesha moja ya dhana ya kilimo (treka) baadhi ya wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maonyesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Mikopo ya dhana za kilimo ni  sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kuwainua wakulima nchini.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...