Search This Blog
Tuesday, July 28, 2020
Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak kukata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 12
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak amesema kuwa atakata rufaa dhidi ya hukumu iliyomkuta na hatia ya ufisadi, na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka 12 jela.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya hukumu ya korti ya juu hii leo, Razak amesema hakuridhishwa na namna mahakama hiyo ilivyohitimisha kesi dhidi yake, na kuongeza kuwa atakata rufaa bila kukawia.
Razak amekutwa na hatia katika mashtaka yote saba ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili, kuhusiana na kashfa ya mabilioni ya dola yaliyokuwa yametolewa na serikali kwa ajili ya mradi wa maendeleo.
Hukumu hiyo ilichukuliwa kama kipimo kwa utawala wa sheria nchini Malaysia, kwani imetolewa miezi mitano tu baada ya muungano unaokijumuisha chama cha Razak kushinda uchaguzi, ambapo wengi walihofu kuwa ushindi huo ungeshawishi uamuzi wa mahakama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment