Search This Blog
Tuesday, July 28, 2020
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeho ameridhishwa na maandalizi kumsindikiza Mzee Mkapa siku ya leo
Na Faruku Ngonyani , Mtwara
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeho amesema kuwa ameridhishwa na maandalizi yaliyofanyika ya kumsindikiza aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo atazikwa siku ya kesho nyumbani kwake kijiji cha Lupaso.
Mabeho amesema kuwa Tanzania tumempoteza kiongozi muhimu kwani enzi za utawala na uhai wake Benjamini Mkapa alihakikisha anapambana na uchumi kwa uweledi na umakini Mkubwa.
Hayati Benjamini Mkapa alifariki Dunia usiku wa tarehe 24 julai 2020 huku sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa aliugua malaria kisha akapata mstuko na kumpelekea kupata umauti.
Tayari mwili wa Marehemu umishawasili Kijiji cha Lupaso huku wananchi wa Wilaya ya Masasi na Viongozi wa Nchi kwa siku ya kesho watapata fursa ya kumsindikza Hayati Benjamini Mpaka katika nyumba yake ya milele.
Hayati Benjamini Mkapa atazikwa katika kijiji hiko cha Lupaso kilichopo Wiliaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
No comments:
Post a Comment