Search This Blog

Wednesday, July 15, 2020

Waziri Mkuu wa Tunisia ajiuzulu na kuitumbukiza Nchi katika mgogoro wa kisiasa


Elyes Fakhfakh alikabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Kais Saied wa nchi hiyo jana Jumatano, ikiwa ni miezi mitano tu baada ya Waziri Mkuu huyo kuunda serikali mpya ya Tunisia, baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba 2019.
Vyanzo vya kisiasa vimedokeza kuwa, Rais Saeid alimuomba Fakhfakh ajiuzulu, wakati huu ambapo Bunge la nchi hiyo lilikuwa kwenye mjadala mkala wa kumtaka Waziri Mkuu huyo aachie ngazi, kwa tuhuma za ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka.
Fakhfakh amekanusha kuhusika na masuala ya ufisadi, lakini kwa wiki kadhaa sasa amekuwepo chini ya mashinikizo kutoka kwa wapinzani waliomtaka ajiuzulu.
Hii ni baada ya mbunge mmoja wa kujitegemea kuchapisha nyaraka mwezi uliopita zinazoonesha kuwa, makampuni ya Fakhfakh yameshinda zabuni zenye thamani ya dinari milioni 44 sarafu ya Tunisia sawa na dola milioni 15 za Kimarekani, kwa kutumia ushawishi wa waziri mkuu huyo serikalini.  


Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, chama cha al-Nahdha chenye mielekeo ya Kiislamu nchini Tunisia kilisema kimevunja uhusiano wake na serikali ya muungano wa vyama kadhaa vya nchi hiyo, kutokana na tuhuma zinazomuandama Waziri Mkuu wa nchi hiyo aliyejiuzulu, Elyes Fakhfakh.
Kabla ya tangazo la jana, Fakhfakh alilieleza bunge la Tunisia kuwa yuko tayari kujiuzulu kama kutatolewa uthibitisho wowote dhidi yake na kusisitiza kuwa, yeye si mmiliki wa makampuni hayo na kwamba ameshauza zamani hisa zake.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...