Search This Blog

Sunday, July 5, 2020

Upendo Nkone: Niliambiwa nimemuua mume wangu, niliumia sana

Mwanamuziki wa injili  ambaye amejipatia umaarufu kupitia nyimbo zake ambazo zimewagusa watu wengi mwana mama Upendo Nkone amefunguka  jinsi alivyoambiwa amemuua mume wake.


"Wakati mume wangu wa kwanza alipofariki sikuwepo nyumbani, katika maisha yangu sikuwahi kuona mtu aliyekufa (maiti) anakuwaje, nilijua tu amelala na ataamka, nilipowaita majirani waliniambia amefariki, ndugu zake walipopata taarifa walisema nimemuua mume wangu, lile jambo liliniumiza sana moyo wangu niliumia sana" Upendo, mwimbaji wa nyimbo za Injili.

"Ruge Mutahaba (The Late) alinipa tuzo moja (Tuzo za Muziki wa Injili) na wakati tuzo hizo zinatolewa sikuwepo nchini, alinipokea yangu anaitwa Franko, nilikuwa safarini Mombasa, kiukweli sikuwa na ukaribu na Ruge, nashukuru sana Clouds kwa kutambua nyimbo zangu" @nkoneupendo, Mwimbaji wa nyimbo za Injili.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...