Katika jitihada za kudhibiti bidhaa zenye viambata vya sumu zinazoagizwa kutoka mataifa ya kigeni, Shirika la viwango Tanzania (TBS) limedhamiria kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote yenye mianya ya njia za panya, ili kukomesha uingizwaji wa bidhaa hizo nchini.
Hatua hiyo inafuata baada ya shirika hilo kukamata shehena ya bidhaa zenye viambata vya sumu kanda ya Ziwa, zikiwa zimehifadhiwa katika maeneo mbalimbali yenye uficho, tayari zikitafutiwa masoko.
Akizungumzia Operesheni hiyo baada ya kuteketeza zaidi ya tani moja ya bidhaa hizo, zinazokadiriwa kugharimu shilingi milioni ishirini, Julius Panga mkaguzi kutoka shirika la viwango Tanzania (TBS) kanda ya Ziwa, anasema zoezi hilo litakuwa endelevu.
Kwa mujibu wa shirika hilo, Operesheni hizo zitakuwa zikiendeshwa usiku na mchana kwa kushirikiana na vyombo vya dola, ili kuhakikisha biashara hiyo na uingizwaji wa bidhaa zenye viambata vya sumu nchini unakomeshwa.

No comments:
Post a Comment