Search This Blog
Friday, July 24, 2020
Takururu Yakamata Mamilioni Uchaguzi Viti Maalum CCM, Mmoja Atupa Hela Chooni
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara inawashikilia watu 5 ambao ni wajumbe wa mkutano wa mkoa wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa wagombea ubunge viti maalumu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Mara, Alex Kuhanda amesema taasisi hiyo licha ya kukamata wajumbe hao pia imekamata kiasi cha Pesa Tsh. 3,300,000 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe ili kuhujumu zoezi la kupiga kura.
Mkuu huyo wa TAKUKURU ameeleza kuwa kwenye kiasi hicho cha fedha kuna Tsh. 70,000 ambayo mmoja wa wajumbe aliitupa chooni baada ya kugundua mtego aliowekewa.
TAKUKURU inatarajia kuwahoji wagombea Ubunge viti Maalum 6 Mkoani Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara wa kutoa rushwa katika Uchaguzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment