Search This Blog

Wednesday, July 22, 2020

Msigwa atoa sababu za kuutosa Urais


Wanachama wanne kati ya 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameingia mitini katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wanachama waliotangaza nia na kutofata fomu ya kuomba ridhaa hiyo ni Msafiri Shabani, Nalo Opiyo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Akizungumza  Mchungaji Msigwa ameeleza sababu za kutoendelea na mchakato wa kuwania Urais kuwa ni wananchi wake walimuomba kuendelea kulitumikia jimbo la Iringa Mjini.
“Sijaingia mitini ila wazee walinifuata wakitaka niendelee kuwatumikia wao pamoja na wana Iringa, hivyo nikaona niachane na Urais nitashiriki wakati mwingine”, amesema Msigwa.
Watia nia waliochukua fomu na kuzirejesha kwa wakati ni aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, Mchungaji Leonard Manyama, Wakili Simba Neo, Wakili Gaspar Mwanalyela, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Lissu na Lazaro Nyalandu.
Leo chama hicho kimeanza mchakato wa kuwachuja wagombea hao ambapo Julai 29 mkutano mkuu utaamua nani atakayekidhi vigezo vya kuipeperusha bendera ya chama katika nafasi ya urais.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...