Search This Blog

Sunday, July 5, 2020

Iraq yalaani Marekani kwa kufanyia jaribio kombora ndani ya ubalozi wake Baghdad


Serikali ya Iraq imeilaani Marekani kwa kufanyia majaribio mfumo wa makombora ya kujihami angani ndani ya ubalozi wake mjini Baghdad.

Naibu Spika wa Bunge la Iraq Hassan Karim al-Kaabi amesema hatua hiyo ni ya kichochezi na ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Aidha ameitaka serikali ya Iraq kuchukua hatua za haraka kusitisha vitendo kama hivyo.

Amesema hatua ya ubalozi wa Marekani kufyatua kombora katika kitovu cha makazi ya raia mjini Baghdad haikubaliki na ni changamoto ambayo inaongeza orodha ya vitendo vya kichochezi na vilivyo kinyume cha sheria vinavyofanywa na Marekani nchini Iraq.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iraq, Marekani imefanyia majaribio mfumo wa makombora wa patriot ndani ya ubalozi wake mjini Baghdad.


Katika miezi ya hivi karibuni hisia dhidi ya Marekani zimeongezeka Iraq tokea jeshi la kigaidi la Marekani lilipomuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Naibu Kamanda wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (Al Hashd al Shabi) mapema Januari mwaka huu mjini Baghdad.

Kufuatia hatua hiyo ya kigaidi ya Marekani, wabunge wa Iraq walipitisha azimio la kutaka wanajeshi wote wa kigeni waondoke Iraq.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...