Search This Blog

Saturday, July 11, 2020

Hospitali mkoani Idlib zafungwa baada ya kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa


Hospitali katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Syria zimesitisha huduma zisizokuwa za dharura baada ya kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona kuripotiwa.

Vile vile, idara inayosimamia elimu imetangaza kufunga shule zote.Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa afya, kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19 kiliripotiwa jana Alhamisi katika mkoa wa Idlib, eneo la mwisho linalodhibitiwa na upinzani .

Daktari aliyekutikana na virusi hivyo tayari amejitenga katika wadi maalum ya hospitali ya Bab al-Hawa huku wagonjwa na wahudumu wengine wa afya aliokaribiana nao wakiwekwa karantini.

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuelemewa kwa mfumo wa afya katika eneo hilo la kaskazini magharibi mwa Syria lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 3.

Vituo vingi vinavyotoa huduma za matibabu vimeharibiwa na vita vya muda mrefu nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...