Search This Blog

Tuesday, June 16, 2020

ZARIF: IAEA haifai kuwa chombo cha kutumiwa na Marekani kuharibu mapatano ya JCPOA


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki haufai kubadilishwa na kuwa chombo cha Marekani kuharibu mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameyasema hayo mjini Moscow Jumanne katika mkutano wa pamoja wa habari na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov. Zarif ameashiria hatua ya Marekani kujiondoa katika mapatano na mikataba ya kimataifa na kusema: "Iran mara zote imekuwa ikionyesha uwazi kamili katika ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na wakala huo na pia  umethibitisha kuwa Tehran imetimiza majukumu yake yote.
Zarif alisisitiza kwamba Iran haifai kuchunguzwa kwa kutegemea nyaraka ambazo ni madai ya kijasusi.

Amesisitiza kuwa, "Iwapo Wakala wa Kimataifa la Nishati ya Atomiki unataka kutumia njia zisizo za kweli, Tehran pia itatoa jibu muafaka."


Waziri wa mambo ya nje wa Iran ameongeza: "Litakuwa jambo la kusikitisha iwapo sekretarieti zaUmoja wa Mataaifa na IAEA zitatumiwa kuangamiza JCPOA.

Zarif amesema yeye na Lavrov wamejadili hatua ya Marekani kukiuka na kupuuza mikataba ya kimataifa. Aidha amesema pia wamejadili kuhusu mazungumzo ya kutafuta amani Syria na kusema viongozi wa Iran, Russia na Uturuki watafanya mazungumzo kwa njia ya video na iwapo hali itaruhusu watakutana ana kwa ana.

Katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov pia amekosia sera za Marekani kuhusu mapatano ya JCPOA na kuongeza kuwa, jitihada za Marekani za kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran hazitafanikiwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...