HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga mwenye uwezo wa kucheza na mpira namna anavyotaka amesema kuwa hawaachi kitu kwenye mechi zote watakazocheza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga imecheza jumla ya mechi 30 kibindoni ina pointi zake 56 imebakiza mechi nane ili kukamilisha mzunguko wa pili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa wachezaji kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
“Tuna mechi ngumu kwenye ligi hilo lipo wazi kwani kwa sasa timu nyingi zinapambana hasa ukizingatia ni lala salama, nasi tuna mipango yetu ya kutoacha kushinda kwenye mechi ambazo tutacheza.
“Kitu cha msingi ni kuona tunakusanya pointi tatu ambazo zitatufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri, hatutaki kumaliza tukiwa nafasi ya tatu tunahitaji ya pili,” amesema Niyonzima.
Kesho, Juni 24, Yanga itamenyana na Namungo, Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment