Search This Blog
Wednesday, June 3, 2020
Watatu mbaraoni DAR kwa kutuhumiwa kumuua dereva UBER
Jeshi polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva taks(uber) aliyefahamika kwa jina la Joseph Mpokala (51) ambaye ni mkazi wa Mbezi kwa Msuguri.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo ,watuhumiwa hao ni Godson Laurent, Sid Mohamed pamoja na Dennis Urassa. Inaelezwa kuwa mnamo Mei 26, 2020 " jeshi la polisi kanda maalumu ilipata taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa mume wake ametoweka tangu Mei 21,2020 na simu zake zote hazipatikani."
Jeshi hilo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari limeongeza kuwa, mnamo Mei 27, 2020 Godson Laurent Mzaura na kuhojiwa kabla ya kukiri kufanya mawasiliano na marehemu ambapo alieleza kuwa mnamo Mei 21 2020 majira ya saa saba mchana walimkodi marehemu ili awapeleke maeneo ya Mbezi na walipofika Mbezi juu watuhumiwa hao walimuua Joseph Tilya na kumfukia kwenye shimo katika eneo la wazi lenye uzio wa ukuta ambao haujamalizika kujengwa .
Aidha baada ya kuhojiwa Juni 1 2020 watuhumiwa wote watatu walihijiwa kwa kina na kukiri kuwa walifanya mauaji hayo na kuchukua gari alilokuwa akiendesha marehemu aina ya IST yenye namba za gari T139 DST na kulificha huko kimara barutri katika numba ya wageni ya Api Forest Lodge.
Hata bhivyo ,jeshi hilo lomesema kuwa linakamilisha taratibu za jalada kwa mwanasheria wa serikali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment