Search This Blog

Monday, June 22, 2020

Watano mbaroni kwa tuhuma za kuhujumu mradi mkubwa wa maji


Wakati Utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora ukiwa tayari umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 baadhi ya wananchi wameanza kuhujumu mradi huo ambapo Jeshi la polisi Mkoa wa Tabora linawashikilia watano kwa tuhuma za kuiba baadhi ya vifaa kwenye mradi huo.

Ni mradi ambao ulisubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Mkoa wa Tabora na viunga vyake na kwamba hadi sasa tayari maji yamekwisha fika katika baadhi ya maeneo ya Mkoa huo jambo la kushangaza mradi huo umeanza kuhujumiwa hata kabla haujakamilika.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuiba pump ya maji yenye thamani ya tsh milioni 32 mali ya Idara ya Maji Wilaya ya Nzega.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...