Search This Blog
Monday, June 22, 2020
Kivuko Kipya cha Rubondo kubeba abiria 50 na magari 6
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi amezindua mradi wa Kiuvuko cha kisiwa cha Rubondo MV kitakachokuwa kinafanya kazi ya kutoa huduma kwa Watalii watakokuwa wakifika kwa lengo la kutalii Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo.
Akizindua Kivuko hicho cha Rubondo MV, kitakachokuwa na uwezo wa kuchuua abiria 50 na Magari 6 kwa wakati mmoja na ambacho thamani yake ni shilingi Bilioni 2.3,amesema hatua hiyo itachangia kufikiwa kwa mpango wa maendeelo wa miaka mitano wa kuongeza idadi ya watalii.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha rubondo ni hifadhi maalum ya utalii kwa ajili ya utalii wa sokwe watu pamoja na utalii wa uvuvi hatua inayodaiwa itachagia kufikiwa kwa malengo ya idadai ya watalii kuongezeka kutoka walitii milioni moja mwaka 2016 hadi kufikia watalii milioni 2 kwa mwaka 2024 hadi 2025. #KilichoBoraKabisa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment