Search This Blog
Tuesday, June 16, 2020
Wanafunzi wa kike elimu ya juu kuwashawishi wakufunzi kwa mavazi yanayoonyesha maumbile
James Timber
Baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu wametajwa kutokuwa na mienendo isiyofaa baada ya kuibuka tabia ya kujirahisi na kuwashawishi wakufunzi kwa mavazi ya yanayoonesha maumbile ili amtamanishe mkufunzi na ajaziwe ufaulu wa hali ya juu bila kujua hiyo ni rushwa ya ngono ambayo inachangia kuleta watumishi wasiofaa kwenye jamii.
Akizungumza kwenye Uzinduzi wa Kongamano la Vunja Ukimya Kataa Rushwa ya Ngono katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Manispaa ya Musoma, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Caroline Mthapula ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo, ameagiza mabinti kuacha mara moja tabia hiyo kwani inawadharirisha wao wenyewe na kuwataka waache mara moja kutumia njia rahisi ya kuweza kufaulu masomo badala yake wasome kwa bidii.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mara Alex Kuhanda ameeleza kuwa wapo makini katika kutokomeza rushwa ya ngono vyuoni kwani wanafunzi wa chuoni wanaandaliwa kuwa watumishi wa kesho ambao wana maadili mema ya kiutumishi .
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Paschal Mahinyila ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa jitihada za kupambana na Rushwa ya ngono chuoni kwake pia kuna changamoto ya aibu kwa wanavyuo kwani wanashindwa kuliongelea sula hilo kwa watu husika wapatapo changamoto hiyo wakihisi wataonekana hawana nidhamu na heshima.
Naye kwa upande wake Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo Frank Peter amemuomba katibu tawala mkoa kushughulikia watendaji wa kata kwani wamekuwa na tabia ya kuwaomba wanachuo rushwa ya ngono wawapo kwenye mafunzo ya vitendo na kutojaziwa maksi ipasavyo kutokana mwanafunzi wa kieke kutompa ushirikiano wa kingono msimamizi wa kiume jamo linalopelekea kufeli kwa wanafunzi wengi wa kike.
Aidha baadhi ya wanafunzi wameeleza kuwa rushwa ya ngono inawaathiri sana watoto wa kike kutokana na kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa na kupoteza masomo yao ikiwa pamoja na wakufunzi kuwapunguzia maksi na kuwafelisha pindi wanapowekewa zuio la rushwa ya ngono.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment