Search This Blog

Sunday, June 14, 2020

Wacongomani wataka sanamu la Leopold II na nembo zote za zama za ukoloni ziharibiwe



Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametaka nembo zote za kikoloni zikusanywe na kuondolewa nchini humo.

Sambamba na kukaribia maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ipate uhuru, raia wa nchi hiyo wametoa wito wa kuondolewa sanamu la mfalme wa zamani wa Ubelgiji, Leopold II kwenye Bustani ya Rais wa Jamhuri mjini Kinshasa.

Mwaka 1885 Mfalme Leopold II alidai kuwa ameinunua Congo na kuifanya milki yake binafsi. Mfalme huyo wa zamani wa Ubelgiji alifanya watu wa Congo kuwa watumwa wake na kuwatumikisha katika kazi za sulubu. Wakoloni hao wa Ubelgiji walikuwa wakikata mikono ya watu walioasi au kukiuka amri yao.


Katika kipindi cha miaka 30 ya ukoloni wake nchini Congo, utawala wa mfalme Leopold II wa Ubelgiji uliua watu milioni.

Mwaka 1967 dikteta wa zamani wa Congo, Mobutu Seseseko aliling'oa sanamu la Leopold II. Hata hivyo serikali ya Joseph Kabila aliyeshika madaraka baada ya Mobutu ililisimika tena sanamu hilo katika bustani iliyoko Kinshasa.

Wiki iliyopita sanamu la Leopold II katika jiji la Antwerp huko Ubelgiji ilichomwa moto, kabla ya mamlaka ya eneo hilo kuiondoa mahala pake. Sanamu nyingine kama hiyo zinazowaenzi wakoloni waliohusika na utumwa na kuwadhalilisha Waafrika zilichafuliwa kwa rangi nyekundu huko Ghent na Ostend na nyingine ikaburutwa chini huko Brussels


Mauaji yaliyofanywa na polisi mzungu dhidi ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd katika mji wa Minneapolis yamechochea maandamano katika kona zote za dunia ambako waandamanaji wanataka kukomeshwa ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa dhidi ya watu weusi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...