Search This Blog
Sunday, June 14, 2020
DC Komba awasukumia TAKUKURU watumishi wa halmashauri
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea apeleke na kukabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) majina ya maofisa na watendaji wa idara ya ardhi ya halmashauri hiyo wakahojiwe ili kufanikisha uchunguzi wa utata wa viwanja vinavyodhani vikuwa vya umma.
Komba alitoa agizo hilo juzi mjini Nachingwea baada ya kukabidhi maghala mawili yenye thamani ya shilingi 360.00 milioni kwa halmashauri ya wilaya hiyo ambayo yameokolewa na TAKUKURU.
Ambayo moja kati ya maghala hayo lilikuwa kwenye mchakato wa kuuzwa kwa shilingi 20.00 milioni wakati thamani ya ghala hilo ni shilingi 280.00 milioni. Huku ghala jingine kati ya maghala hayo yaliyokuwa mali ya Shirika la Maendeleo ya Nachingwea(SHIMANA) lenye thamani ya shilingi 78.00 lilitwaliwa na chama cha msingi cha ushirika(AMCOS) bila kufuata taratibu.
Alisema nijambo lisiloingia akilini serikali ambayo ilipima eneo lililojengwa maghala hayo kuweka kiwanja ambacho kimejengwa kituo cha mafuta. Huku akionesha wazi mashaka kwamba hata kiwanja kilichojengwa kituo hicho ni miongoni mwa viwanja vilivyopatikana kutoka kwenye eneo la lililokuwa SHIMANA.
'' Nakumbuka mkuu wa TAKUKURU umenieleza kwamba nyuma ya maghala zimetengenezwa kona utadhani hakijapimwa na serikali.
Nakubali maelezo yako kwamba ramani ya eneo hili imechezewa na wametengeneza ramani nyingine ili kubana eneo na kupata viwanja vingine. Sasa mimi namuagiza mkurugenzi akuletee majina ya maofisa wa idara ya ardhi ili mtakapowahitaji awe anawaruhusu,'' Komba alizidi kuwaweka roho juu maofisa na waliojenga jirani na maghala hayo.
Komba licha ya kutoa wito kwa TAKUKURU ikaze kamba ili eneo lote la maghala lirudi mikononi mwa umma alizidi kuichambua idara hiyo kwamba wananchi wanadhulumiwa sana na watumishi wa idara hiyo wasio waadilifu. Huku ikisababisha migogoro ya mara kwa mara.
'' Wananchi wanadhulumiwa sana, kuna mtu amelipa shilingi milioni tisa hajaoneshwa wala kupewa kiwanja. Badala yake anapigwa danadana na kumsumbua kufuatilia kwenda na kurudi,'' Komba alizidi kuwakalia kooni.
Alipongeza TAKUKURU kwa kuokoa maghala hayo. Ambayo moja lenye thamani ya shilingi 280,000,000 lilikuwa kwenye mpango wa kuuzwa kwa shilingi 20,000,000.
Huku jingine lenye thamani ya shilingi 78,000,000 likiwa limetwaliwa na chama cha msingi cha ushirika(AMCO) bila kufuata taratibu.
Alibainisha kwamba kama TAKUKURU isingeingilia kati hakuna mali ambayo ingekuwa salama kuanzia majengo hadi eneo.
Huku akiweka wazi kwamba hiyo inatoa somo kwa taasisi za kiuchunguzi zilizo ndani ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya zitimize wajibu wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment