Search This Blog
Thursday, June 11, 2020
Vikwazo vya kukaririwa vya Marekani dhidi ya Iran na kufeli mtawalia kwa sera za Washington
Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Marekani ilianza kutekeleza vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu ikiwa na lengo la kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kisha kuilazimisha kuketi kwenye meza ya mazungumzo.
Mafanikio ya Iran katika kusimamia uchumi, kukabiliana na kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona katika kilele cha vikwazo vya Marekani, na muhimu zaidi kuelekea na kuwasili salama huko Venezuela meli tano kubwa za mafuta ya petroli kutoka Iran, kivitendo vimetoa changamoto kubwa kwa sera za mashinikizo ya kiwango cha juu na vikwazo vya upande mmoja za Marekani.
Marekani inafanya kila iwezalo kuitwisha Iran matakwa yake kupitia njia ya kuzidisha vikwazo katika sekta mbalimbali; hata hivyo kusimama ngangari kwa taifa na serikali ya Iran kumewafanya viongozi wa Marekani wakariri vikwazo hivyo. Katika hatua ya hivi karibuni zaidi, Marekani imeyawekea vikwazo makampuni matano ya meli ya Iran baada ya Jamhuri ya Kiislamu kutunisha misuli baharini na kuingia kwenye maji ya Venezuela baada ya kupita jirani na Marekani.
Suala hili la kudhihirisha udhaifu wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran kwa misimamo na maamuzi makini ya Tehran linapaswa kupewa mazingatio maalumu, na hatua kama hizo zinatoa ujumbe kwa viongozi wa serikali ya Washington kwamba, Jamhuri ya Kiislamu kamwe haitapiga magoti mbele ya mashinikizo ya kiwango cha juu na vikwazo vya kukaririwa vya Marekani.
Katika uwanja huo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Sayyid Abbas Mousavi alisema kuhusiana na vikwazo vya sasa vya Marekani dhidi ya makampuni 5 ya meli za mafuta ya Iran kwamba: "Maafisa wa Marekani wanajisumbua wao wenyewe kwa kuweka vikwazo vya kukaririwa, na Iran haitasalimu amri kwa vikwazo na mashinikizo kama hayo."
Mchezo wa Marekani wa kutumia silaha ya vikwazo dhidi ya Iran umefeli kivitendo na jihudi zinazifanywa na Washington katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kudumisha vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu zitakumbwa na hatima hiyo hiyo.
Baada ya kushindwa kuiburuta Iran kwenye meza ya mazungumzo kupitia njia ya vikwazo vya kiwango cha juu ili kuimazimisha makubaliano mbadala ya yake ya JCPOA, sasa Marekani inafanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba, inaharibu kabisa makubaliano hayo yenyewe ilhali si mwanachama tena katika makubaliano hayo. Harakati hii imekabiliwa na upinzani wa China, Russia na nchi za Ulaya na sasa Washington inakabiliana uso kwa uso na irada na azma ya kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alisema katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hapo tarehe 7 mwezi huu wa Juni kwamba: "Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Marekani haina tena haki ya kuwasilisha mashtaka dhidi ya Iran kwa mujibu wa makubaliano hayo."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment