Search This Blog

Tuesday, June 2, 2020

Vifo vya Ebola vyaongezeka DRC


Idadi ya vifo kutokana na Ebola imeongezeka na kufikia watu watano  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kulingana na ripoti ya UNICEF mtu mmoja mwingine amepoteza maisha kutokana na Ebola Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Watu wanne walioambukizwa wametengwa katika Hospitali ya Wangata katika mkoa huo.

Watu 4 wamepoteza maisha  jana kutokana na ugonjwa huo.

Waziri wa Afya wa DRC Eteni Longonda ameomba ushirikiano wa Shirika la Afya Ulimwenguni, akitangaza kwamba janga hilo limetokea tena katika mkoa wa Mbandaka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...