Search This Blog

Thursday, June 18, 2020

Serikali yazindua kituo cha Taifa cha tiba mtandao


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu amezindua kituo maalum cha Taifa cha Tiba Mtandao (Teleradiology) katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kitakachosaidia kusogeza huduma za Kibingwa kwa Wananchi kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Taasisi ya MOI jijini Dar Es Salaam Waziri Ummy Mwalimu amesema Kituo hicho cha huduma za Matibabu ya Kibingwa kilichounganisha Hospitali 13 kitasaidia kupunguza gharama za nauli kwa wananchi kuzifikia huduma za kibingwa na kuwataka watendaji wa Wizara ya Afya pamoja na Taasisi zingine zilizobuni mradi huo kuharakisha mchakato wa kuzifikia Hospitali nyingi zaidi ikiwemo hospitali zote za rufaa za Serikali, za Halmashauri pamoja na vituo vya Afya.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...