Search This Blog

Sunday, June 28, 2020

SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMELETA MAENDELEO PWANI- MHANDISI NDIKILO

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema ndani ya miaka mitano chini ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli imepata maendeleo makubwa sana.

Ndikilo amesema, toka kupata kwa Uhuru mji wa Kisarawe haujawahi kupata maji safi na kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam  DAWASA wamefanikisha kukamilika kwa mradi huo.

Mradi wa maji wa Kisarawe umeuzindulia leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli, tunafurahi sana kwa maji kupatikana ndani ya mji huu na pia kuna miradi mingi ya maji ndani ya mkoa wa Pwani.

Ndikilo, amesema Mkoa wa Pwani umefanikiwa kukusanya mapato ya Shilingi Bilion 53 ikiwa ni ongezeko kubwa katika kipindi cha miaka mitano.

Amesema, toka kuingia serikali ya awamu ya tano imeleta maendeleo makubwa, ikijenga Hospitali za Wilaya katika halmashauri zote tisa.

Mbali na hilo, Ndikilo ameeleza kuwa awali Mkoa wa Pwani ulikua unategemea kilimo cha Korosho na Ufuta ila kwa sasa wameongeza zao la Katani na kilimo cha miwa sambamba na kuanzisha kiwanda kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari.

Pia, Mkoa wa Pwani umepiga hatua kwa viwanda mbalimbali kuanzishwa ikiwemo Kiwanda cha nyama cha Tanchoice kilichopelekewa maji kwa mradi wa Bilioni 1.2
Rais Dkt John Pombe Magufuli wa pili kulia akizindua mradi wa Maji Kibamba Kisarawe uliojengwa kwa gaharama zaidi ya shilingi Bilioni 10.6,katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wameshiriki.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...