Search This Blog
Wednesday, June 3, 2020
Mtoto wa Miaka Miwili Auliwa kwa Kushambuliwa na Fisi
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili, Charles Makilika amaeuliwa baada ya kushambuliwa na fisi usoni katika kitongoji cha Mwagala, Ugweto Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza na vyombo vya habari jana Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Juni 01, 2020 majira ya saa moja jioni wakati mtototo akicheza na wenzake.
“Wakati anacheza na wenzake gafla alitokea na kumshambulia usoni kwa kumng’ata na kumburuza umbali wa mita 50 na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza uhai.
Aidha, Kamanda amewataka wananchi kuhakikisha watoto wanacheza katika eneo ambalo ni salama hasa kipindi hiki fisi wamezagaa katika maeneo mbalimbali.
Mpaka sasa kuna matukio sita ya watu kujeruhiliwa na fisi na watoto watatu wakipoteza maisha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment