Search This Blog

Sunday, June 21, 2020

Msauzi amuondoa Tshishimbi Yanga

By KHATIMU NAHEKA

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi hatacheza mechi dhidi ya Azam kesho na hata ya Namungo Jumatano kuna hatihati.

Tshishimbi alikuwa anafikiri angeweza kucheza mchezo huo na tayari alishajiandaa lakini mmoja wa watalaam wa kigeni katika benchi lao amemzuia akimwambia atulie bado kidogo.

Taarifa ya kitabibu iliyotolewa na daktari mkongwe wa timu hiyo, Shecky Mngazija ni kwamba nahodha huyo amezuiwa na mtaalam wa tiba ya viungo Fareed Caseem.

“Tshishimbi hataweza kuwa tayari kwa mchezo huo. Kuna maelekezo mapya yametolewa na daktari mwenzangu wa tiba ya viungo kwahiyo hatacheza,” alisema Mngazija.

Mngazija aliongeza kuwa Caseem, raia wa Afrika Kusini anataka kuona anapona vizuri kabisa.

“Anachotaka (Caseem) ni kuona Tshishimbi anapona kabisa ili akirudi awe sawa ndio sababu kubwa ya uamuzi huu na tayari tumeshawapa taarifa makocha kwa hatua nyingine za kikazi,” alisema Dk Mngazija.

Advertisement

Baada ya taarifa hizo Mwanaspoti ilimtafuta nahodha huyo ambaye alionyesha kuumizwa na akisema amelazimika kuwaelewa madaktari wake.

“Nilikuwa nadhani ningeweza kucheza, lakini nilipokutana na madaktari wameniambia hivyo kwamba nitakuwa nje kwa muda zaidi,” alisema Tshishimbi.

“Unajua nilipanga mengi katika mchezo huu wa Azam, nilitaka kuona tunaishusha rasmi Azam pale juu lakini naona Mungu hakupenda nicheze. Nitazungumza tu na wenzangu kuwahimiza juu ya umuhimu wa ushindi katika mchezo huu.”

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...