Search This Blog
Thursday, June 11, 2020
Mkuu wa majeshi aomba msamaha kwa kwenda kanisani na Trump
Mkuu wamajeshi nchini Marekani amekiri kuwa alikosea kuungana na Rais Donald Trump wakati wa alipotembea kuenda kanisa lililopo karibu na Ikulu ya Marekani ambalo liliharibiwa na waandamanaji.
Tukio hilo la Juni tarehe moja na ambalo lilizua utata lilionesha "taswira kwamba jeshi linajihusisha na siasa za ndani ya nchi", Jenerali Mark Milley alisema.
Bwana Trump alitembea hadi kanas hilo na kupiga picha akiwa ameshikilia Bibilia baada ya maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd kuvunjwa kwa nguvu.
Kwanini viongozi wa makanisa wamekasirishwa na Trump?
Trump 'hakufuata' katiba, asema mkuu wa zamani wa jeshi
Hatua ya kutumia wanajeshi kukabiliana na waandamanaji imezua mjadala mkali cnini Marekani.
Trump mara kwa mara alitumia maneno "Utawala wa sheria", kuleta kikosi malum cha ulinzi katika mji mkuu wa Marekani, na kuapa kuwa atawapeleka wanajeshi katika miji mingine ya Marekani huku akilaani maandamano ya vurugu yaliyoshuhudiwa nchini humo.
Baadhi ya maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd mjini Minnepolisi mwezi uliyopita, mwanzoni yalikuwa ya amani lakini baadaye yalikumbwa na vurugu na wiz katika miji tofauti.
Lakini tangu maafisa wanne waliohusika na mauaji hayo kufunguliwa mashitaka, maandamano hayo yamekuwa ya amani, huku wanaharakati wa kimataifa wakiungana kupinga mateso ya polisi na ukosefu wa usawa katika jamii.
Kanda ya video ya mauaji ya Minneapolis inaonesha afisa wa polisi mzungu akipiga goti katika shingo ya Bwana Floyd kwa karibu dakika tisa.
Jenerali Milley amesema nini?
Mkuu huyo wa majeshi alikuwa akizungumzia kuhusu video hiyo wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Chuo Kikuu cha Ulinzi nchini.
Alisema: "Sikustahili kuwa hapo. Uwepo wangu hapo wakati wa tukio hilo ilionesha taswira kwamba majeshi yanajihusisha na siasa za ndani ya nchi.
"Kama afisa mkuu wa majeshi ilikuwa makosa na nimepata funzo, natumai nimejifunza kutokana na tukio hilo."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment