Search This Blog
Wednesday, June 3, 2020
Jeshi la Polisi Linamshikilia Mwanamke Aliyekutwa na Pembe ya Ndovu Yenye Thamani ya Sh milioni 34
Mwanamke Nuru Hassan (35) mkulima na mkazi wa kasiki Wilayani Kilosa mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Juni 01, 2020 majira ya saa 1:00 asubuhi katika kitongoji cha Ksiki tarafa na wilaya ya Kilosa.
Amesema askari polisi kwa kushirikiana na askari wanyamapori wa hifadhi ya Mikumi wakiwa kwenye doria walipokea taarifa za kuwepo kwa mtu mwenye nyara za serikali na walipofuatilia ndipo walimbaini mwanamke huyo.
Kamanda amesema baada ya kupokea taarifa hizo askari hao walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Amesema baada ya upekuzi ndani ya nyumba yake walikuta pembe moja ya ndovu yenye uzito wa kilo 7.5 yenye thamani ya Sh 34,635,00
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment