Search This Blog
Wednesday, June 17, 2020
Hawa ndio 11 walioomba kupitishwa Urais CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo Juni 17, 2020, kimetangaza majina ya Wanachama wake 11 walioomba kuteuliwa na Chama hicho kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.
Majina hayo yametajwa leo ambapo imesisitizwa kuwa mchakato wa awali ulikuwa unahusisha kuandika barua ya kitia nia na sio kuchukua na kurudisha fomu, hivyo watu walioandika barua kwa Katibu Mkuu John Mnyika ni 11.
Wanachama hao wametajwa akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na Peter Msigwa.
Wengine ni kada wa zamani wa CCM na mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Mwita Isaya, Dkt Majinge Mayrose, Manyama Leonard, Nicodemus Gasper, Nalo Opio, Neo Richmond na Shaaban Msafiri.
Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa kuna baadhi ya wanachama ambao wameelezwa kuwa ni bodaboda walijikusanya na kumwandikia barua mtu mmoja (ambaye hajatajwa) ili agombee lakini barua yao haikukidhi vigezo kutona na kuwepo kwa sharti la mtu mwenyewe kuandika barua na sio kuandikiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment