Search This Blog
Monday, June 15, 2020
Freeman Mbowe Ajitosa Kugombea Urais wa Tanzania
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe jana Juni 15, 2020, ameandika barua ya kutia nia kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Mbowe ametia nia hiyo jana Jumatatu tarehe 15 Juni 2020 baada ya kupelekewa barua iliyoandikwa na baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wa chama hicho ili aisaini na kupelekwa Ofisi ya Katibu Mkuu.
Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, amepelekewa barua hiyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, anakoendelea kupata matibabu baada ya kudaiwa kushambuliwa usiku wa kuamkia tarehe 9 Juni 2020.
Hatua ya Mbowe kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, kinazidisha joto la urais ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.
Joto hilo, linatokana na waliokwisha kujitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa na ushawishi ndani ya chama hicho hivyo kukipa wakati mgumu kumpata mmoja.
Wengine waliokwisha jitosa ni; Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Tundu Lissu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu na mwanachama wa chama hicho, Dk. Maryrose Majige.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment