Search This Blog

Thursday, June 4, 2020

Ajibu arejeshwa Simba kwa masharti

By THOBIAS SEBASTIAN

MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib amerudishwa katika kambi ya timu hiyo na Jumatatu jioni alikumbana na tizi la nguvu katika mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa Mo Bunju Arena.

Ajib alitimuliwa kambini hivi karibuni na kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck huku akiwa na mabegi yake mgongoni kwa kosa la kuchelewa kuripoti, lakini moja ya masharti aliyopewa baada ya kurejeshwa ni kujituma sana kimchezo na kujirekebisha kinidhamu huku faini ikimhusu pia.

Adhabu ya Ajib imemalizika lakini ni sharti alipe faini ya Sh200,000 ambayo atakatwa katika mshahara wake mwisho wa mwezi Mei kama sehemu ya utaratibu wa nidhamu wa Simba.

Juzi Jumatatu asubuhi Ajib alifika kambini, Mbweni na kuzungumza na Sven mazungumzo mafupi kisha aliruhusiwa kuwa sehemu ya wachezaji na maisha yakaendelea.

Mwanaspoti lilikwenda kuweka kambi katika mazoezi hayo ya Simba, juzi jioni na kumuona Ajib akiwa katika kikosi cha wachezaji wa Simba ambao walifanya mazoezi katika uwanja huo.

Katika mazoezi hayo Ajib alikutana na cha moto baada ya mazoezi kuanza saa 11:00 jioni kwani alikimbizwa mbio za kuzunguka uwanja huku Sven akiwa anamsimamia.

Advertisement

Ajib akiwa anakimbia mbio za kasi na polepole akizunguka uwanja mzima, Sven alikuwa akimsimamia huku wachezaji wengine wote wakiwa katikati ya uwanja wakiwa wanafanya mazoezi ya kawaida.

Mazoezi hayo ya kawaida kwa wachezaji wengine yalikuwa yakisimamiwa na kocha wa viungo, Adel Zrane aliyekuwa sambamba na kocha msaidizi Selemani Matola.

Mchezaji huyo hakuwa anakimbia mwenyewe bali alikuwa na wachezaji wengine Rashid Juma na Francis Kahata ambaye naye alikuwa anafanya mazoezi ya kwanza ya uwanjani akiwa na kikosi hicho tangu aliporejea nchini.

Sven alionekana kumkadhania Ajib na kumkomalia kutaka akimbie kwa kasi kama vile ambavyo alikuwa anataka mwenyewe na muda wote macho yalikuwa kwake.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...