Search This Blog

Friday, May 1, 2020

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI UJENZI ZAHANATI


~ Kuwaondolea kero ya afya
~ Waridhishwa na ujenzi
 
Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Wananchi wa Kijiji cha Miuta kata ya Miuta wamemshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kuwajengea Zahanati ya Miuta ambayo inaenda Kuwaondolea kero ya kupata huduma ya afya. 

Wananchi hao ambao awali wameridhishwa na kasi na kiwango cha ujenzi wa Zahanati hiyo wameomba Zahanati hiyo ikamilishwe vyema ili ianze kutoa huduma za afya na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kusaka huduma za afya. 

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kutujengea Zahanati hii ya Miuta, sisi Wanakijiji cha Miuta tunampongeza kwa kutujali. Tunaomba kituo kikamilishwe vyema na kianze kutoa huduma za afya ili kutuondolea adha ya kupata huduma mbali za afya.” Alisema Juma Akili Mohamed almaarufu Fundikira. 

Wananchi hayo waliyasema hayo kwenye ziara aliyoifanya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ya kutembelea mradi huo ambapo Wananchi hao walimuomba Afisa Tarafa huyo afikishe salaam zao za shukrani na za upendo kwa Rais Magufuli aliyewajali Wanyonge wa Miuta kwa kuwajengea Zahanati hiyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...