Search This Blog

Monday, May 25, 2020

Waislamu kote duniani washerehekea Idd ul fitri chini ya vizuizi vya kukabiliana na corona


Waislamu kote duniani wanasherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr huku wengi wakiwa chini ya vizuizi vilivyowekwa na mataifa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.

 Sherehe hizo zimeandamwa na kiwingu cha janga la corona huku nchi nyingi duniani zikitangaza kurejesha vizuizi ambavyo kwa sehemu vililegezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika hali ya kupunguza msisimko wa sherehe hizo mataifa kadhaa ikiwemo Saudi Arabia, Uturuki, Misri na Syria yamepiga marufuku ibada za umma, moja ya tukio muhimu katika sikukuu ya Eid, kwa lengo la kuzuia kusambaa virusi vya corona.

 Sikukuu ya Eid huashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramdhan na huadhimishwa kwa ibada ya swala, dhifa za chakula na manunuzi ya zawadi pamoja na mavazi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...