Licha ya uwepo wa janga la Corona, tuzo za BET 2020 ambazo ni tuzo za 20 tangu kuanzishwa kwake, sasa rasmi zatangazwa kuwa zitafanyika ila kwa namna ya pekee.
Kupitia taarifa iliyotolewa na waandaaji wa tuzo hizo wametoa tamko la kuendelea na programu hiyo ambayo itafanyika Juni 28 mwaka huu.
Kwenye usiku wa tuzo hizo pia kutakuwa na hafla ya kusherehekea miaka 40 ya kuanzishwa kwa kituo cha BET (Black Entertainment Television), kulingana na kanuni za kuepusha mikusanyiko, BET wametangaza kuifanya hafla hiyo katika namna ya "Virtually" kama kitaalamu inavyoitwa.
Hii ni namna ambayo itatumia njia za kibunifu za Kiteknolojia pamoja na maudhui ambayo yatatengenezwa na wasanii wenyewe ili kumfanya mtazamaji na hata msanii na wadau wengine wajihisi kama wapo pamoja ukumbini.
Aidha, #BET hadi sasa bado hawajaweka wazi majna ya wasanii washiriki kwenye tuzo hizo za mwaka huu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment