Search This Blog
Wednesday, May 6, 2020
Spika Ndugai Awataka CHADEMA Wajiandae Kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu
Spika wa Bunge ,Job Ndugai amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Tundu Lissu.
Spika Ndugai amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.
“Nimepata nakala ya hukumu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hio wajiandae kulipa ” amesema Spika Ndugai
Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama cha Mapinduzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment