Search This Blog
Wednesday, May 6, 2020
Kimenuka...Spika Ndugai Awataka Wabunge Wote CHADEMA Waliosusia Vikao Vya Bunge Warudishe Mamilioni Ya Pesa Walizolipwa
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa Chadema waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni
Spika ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.
"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1 - 17 Jumla ya zaidi Sh Mil 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh Mil 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Mil 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa; "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment