Search This Blog

Thursday, May 14, 2020

Sababu ya ndoa ya Haji Manara kuvunjika, yatajwa



OFISA Habari wa Simba, Haji Manara  amesema kuwa ameachana na mkewe na tayari ameshaolewa kutokana na presha kubwa kutoka kwa familia ya upande wa mke wake.

Manara amesema kuwa ana mpango wa kuoa mke mwingine ambaye atakuwa mzuri huku suala la tabia akiliweka kando kidogo.

" Kulikuwa kuna presha kubwa sana upande wa mke wangu hadi nikafikia kuamua kuachana naye.Siku chache baadaye nikasikia ameolewa, wala sikushituka kwa kuwa hili nilijua lilikuwa limeandaliwa na linakwenda kuwa hivi.

 “Kwa sasa nasubiri kwanza lakini nitaoa na mwanamke ninayetaka kumuoa lazima awe mrembo sana. Nataka mwanamke mrembo hasa, suala la tabia litafuatia.”



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...