Search This Blog

Sunday, May 17, 2020

Obama akosoa hatua za kushughulikia janga la virusi vya corona



Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameikosoa serikali ya Trump kuhusu jinsi inavyoshughulikia janga la virusi vya corona wakati wa hotuba yake kwa wanafunzi waliohitimu kutoka vyuo vya elimu na vyuo vikuu hapo jana.

 Hata hivyo hakumtaja rais wa sasa Donald Trump ama afisa yeyote mkuu wa Marekani katika hotuba yake ya ufunguzi kwa wanafunzi hao lakini alisema kuwa kuna ukosefu wa uongozi katika mzozo huo.

 Wakati huo huo, gavana wa jimbo la New York Andrew Cuomo, amesema kuwa visa vipya vya maambukizi katika jimbo hilo vinatokana na watu wanaofanya ununuzi, mazoezi ama wanaojumuika pamoja kutokana na kulegezwa kwa vikwazo dhidi ya virusi hivyo. Jimbo la New York limeanza kufuatilia watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona hatua inayotarajiwa kuwahusisha mamia ya watu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...