Search This Blog
Sunday, May 17, 2020
Neno la Ndugulile baada ya Mollel kuteuliwa
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile ameeleza kushukuru uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli juu ya kumtengua na nafasi yake kuijaza Mbunge wa Siha,Godwin Mollel.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ndugulile ameandika ujumbe pia wa kumpongeza Dkt. Godwin Mollel kwa kupewa nafasi hiyo.
"Nimepokea uamuzi wa Rais Magufuli kwa unyenyekevu mkubwa, ninamshukuru sana kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. nawashukuru sana Ummy mwalimu na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia, namtakia kila la kheri Naibu Waziri ajaye Dkt. Godwin Mollel." Faustine Ndugulile aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya."
Jana Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile na kumteua Godwin Mollel ambaye ni Mbunge wa Siha kushika nafasi hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment