Search This Blog
Monday, May 11, 2020
NIGERIA: Hoteli zavunjwa kudhibiti maambukizi ya corona
Maafisa nchini katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers nchini Nigeria wamevunja hoteli mbili kufuatia madai ya kukiuka sheria za kukaa nyumbani zilizowekwa kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.
Gavana wa jimbo hilo Nyesom Wike, ambaye alisimulia kuvunjwa kwa Hoteli ya Edemete Hotel na Prodest Home Jumapili, alisema kuwa waliofanya shughuli hiyo walikuka maagizo kwamba hoteli zinapaswa kufungwa.
Alisema kuwa watu waliopatikana na virusi vya corona walipatikana katika hoteli mbali mbali katika jimbo hilo. Lakini hakusema iwapo yeyote ambaye ana maambukizi ya Covid-19 amekuwa akiishi katika hoteli hizo mbili zilizovunjwa.
Mameneja wa hoteli zote mbili wamekamatwa, lakini mmiliki wa Prodest Home amekana kwamba hoteli yake ilikua imefunguliwa.
"Hoteli haikua ikifanya kazi na 70% ya wahudumu walikua wamerudishwa nyumbani ," Gogorobari Promise Needam alioiambia BBC.
"Kulikua na watu watatu tu katika hoteli.
"[Maafisa ] walikuja na walikua wakiomba rushwa wakasema watatuacha tuendelee kufanya kazi, kama tutawapatia pesa lakini tukawambia hatufanyi kazi kwa hiyo hatuna pesa za kuwapatia ," alisema .
Serikali ya jimbo la Rivers amekanusha shutuma hizo.
Jimbo hilo kwa sasa lina jumla ya visa 15 vya maambukizi ya virusi vya corona na imerekodi vifo viwili.
Amri ya kukaa nyumbani iliwekwa katika mji mkuu wa jimbo hilo, Port Harcourt, Alhamisi iliyopita.
Nigeria ina zaidi ya visa 4,300 vilivyothibitishwa vya virusi vya corona, huku mji mkuu wa biashara wa Lagos ukiwa ni kitovu cha maambukizi.
Lakini sharia ya kukaa nyumbani ambayo iliwekwa huko, na katika baadhi ya majimbo mengine, mwezi Machi ililegezwa.
Wataalamu wa sheria wameiamba BBC kuwa hatua zilizochukuliwa katika Rivers na gavana wa jimbo zinaweza kupingwa mahakamani.
akini serikali ya jimbo inasema kuwa Bwana Wike alisaini sheria ya kumpa mamlaka ya kutekeleza amri ya kukaa nyumbani.
Jimbo hilo limekua likikosolewa kwa kuweka sheria kali za kukaa nyumbani, ambazo zinaamuru masoko, na maeneo ya kuuza chakula kufungwa.
Madaktari, mafamasia na wafanyakazi wengine wa kazi muhimu pia wameripoti kuwa wamekua wakinyanyaswana wakati mwingine kukamatwa kwa kukiuka sheria ya kukaa nyumbani.
Maafisa wameweka vizuizi katika barabara kuu katika mpaka wake wa mashariki ili kuimarisha marufuku ya usafiri baina ya majimbo ,wakiwashutumu maafisa wa usalama kwa kuwaibia watu nyakati za usiku.
Maafisa pia wanapanga kufanya mnada wa kuuza magari yaliyokamatwa kutoka kwa wale wanaokiuka amri ya kukaa nyumbani.
Ni wale tu waliopokea vibali maalumu, vilivyotolewa na gavana mwenyewe wanaoruhusiwa kutembea.
Lakini, inaonekana wale waliomo katika serikali pekee ndio wenye waraka unaoelezea ni vipengele gani hasa kwani wakazi wa jimbo hilo wameiambia BBC kuwa hawaielewi.
Maafisa wa jimbo hilo hawakujibu BBC walipoombwa kuwasilisha nakala ya sheria hiyo.
Wakili Ahmed Abass aliiambia BBC kwamba sheria hiyo ya gavana haiwezi kumpa mamlaka ya kuvunja jengo.
"Sheria ya amri huundwa na rais au gavana kwa kuzingatia sheria zilizopo nchini," alisema na kuongeza kuwa haiwezi kwenda zaidi ya katiba, ambayo inatoa fursa ya kesi huru.
"Kile ambacho [Bwana Mike] alipaswa kufanya ni kuwakamata wamiliki wa hoteli, awapeleke mahakamani na wangeshitakiwa ," aliiambia BBC.
Alielezea matendo ya gavana kama "utendaji wa kizembe na matumizi mabaya ya ofisi ".
Nigeria ina mfumo wa utawala wa shirikisho na majimbo hubuni sheria fulani kwa ajili ya masuala yanayoyahusu.
Bwana Wike binafsi alizunguka binafsi katika siku za mwanzo za amri ya kukaa nyumbani kufuatilia iwapo sheria hiyo inatekelezwa na akasema kuwa aliridhika jinsi watu wanavyoheshimu maagizo wanayopewa.
Katika tukio moja, alichukuliwa picha ya video akiamuru kukamatwa kwa watu wawili barabarani na akaagiza wapelekwe mara moja kwenye kituo cha kujitenga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...




No comments:
Post a Comment