Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imejizatiti na imejipanga kuhakikisha kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni pamoja na kuzingatia masharti ya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mhe.Jaji Semistocles Kaijage katika kikao na vyama vua Siasa na Wadau wengine wa Uchaguzi kujadili na kupitisha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2020.
Akizungumza katika kikao hicho Jaji Kaijage amesema kuwa NEC kwa kushirikiana na vyama vya Siasa na Serikali huandaa Maadili ya Uchaguzi kwa shabaha ya kuwa Uchaguzi ulio huru, wa haki, wa wazi na wa kuaminika.
“Maadili yatasaidia kuwa na uwanja sawa wa ushindani katika Uchaguzi.Maadili hayo huandaliwa kwa mujibu wa kifungu Cha 124A Cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya sheria za Tanzania kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo”. Amesema Jaji Kaijage.
Jaji amesema kuwa ni muda mwafaka tena kwa vyama vya siasa, Tume na Serikali kama wadau wa Uchaguzi kuandaa Maadili hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
“Natambua kuwa vyama na Serikali mlipewa Rasimu ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 ambapo mlipata fursa ya kupitia na kutoa maoni na mapendekezo yenu ambayo yamezingatiwa katika Rasimu hii ya Maadili”. Amesema Jaji Kaijage.
Pamoja na hayo Mhe.Kaijage aliwaaomba Wadau mbalimbali wa Uchaguzi baada ya majadiliano hayo na kuridhiwa kwa Maadili,wahusika wataweka saini ya kuyakubali, kuyaheshimu na kuyatekeleza kuanzia wakati was kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na chaguzi ndogo zitakazofuata.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment