Search This Blog
Wednesday, May 27, 2020
Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Rwanda akanusha tuhuma dhidi yake
Felicien Kabuga, mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ambaye alikuwa mafichoni kwa muda wa miaka 26 kabla ya kukamatwa siku chache zilizopita nchini Ufransa amekanusha mashitaka ya kuhusika na mauaji hayo.
Kabuga mwenye umri wa miaka 84 jana Jumatano kupitia mkalimani aliimbia Mahakama ya Ufaransa kuwa, "yote haya ni urongo, sijaua Watutsi wowote, nilikuwa nafanya kazi nao."
Mshukiwa huyo anaandamwa na makosa saba yakiwemo ya uchochezi wa mauaji ya kimbari, jinai dhidi ya binadamu na kuunda na kufadhili kundi la wanamgambo wa kikabila ambalo lilitekeleza mauaji hayo ya kimbari ya 94.
Hapo jana pia, mahakama hiyo ya Ufaransa ilikataa kumuachia huru Kabuga. Mawakili wake walikuwa wameiomba mahakama hiyo imuachie huru kwa dhamana kutokana na hali yake mbaya ya kiafya na imuwekea chini ya uangalizi wa korti.
Mtuhumiwa huyo mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda alikamatwa na polisi mjini Paris mapema mwezi huu, baada ya kuukwepa mkono wa sheria kwa zaidi ya miaka 26.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment