Search This Blog

Monday, May 4, 2020

Mambo manne yaiweka shakani Ligi Kuu England

London, England. Frank Lampard ametaja mambo manne makubwa ambayo yanaweza kuiweka katika mazingira magumu Ligi Kuu England endapo itarejea.

Kocha huyo wa Chelsea ametoa kauli hiyo huku tarehe rasmi ya kuanza mashindano hayo ikiwa bado kitendawili.

Mashindano yote yamesimamishwa kutokana na janga la corona, lakini baadhi ya ligi zinaweza kuendelea endapo maambukizi ya virusi vya corona yatapungua.

Lampard alisema ligi haiweza kuanza kama kutakuwa na idadi kubwa ya maambukizi jambo linaloweza kutishia afya za wachezaji na maofisa.

“Sina nina ya kumnyoshea mtu kidole kwasababu wote tuna lengo moja tunataka ligi irejee.

Advertisement

Ni vyema kabla ya ligi kuanza kama itakuwa Juni 12 au kucheza bila mashabiki, lakini jambo la msingi ni kupima afya za wachezaji na maofisa kabla ya mashindano kuanza,”alisema Lampard.

Alisema umakini unatakiwa katika uchuakuji wa vipimo hasa kwa makofisa na wafanyakazi ambapo baadhi ya klabu zina watu wengi akitolea mfano Chelsea yenye wafanyakazi kati ya 70 hadi 80.

Pia alizungumzia namna bora ya wachezaji katika kufanya mazoezi bila kugusana baada ya timu zote kukubaliana kuanza kujifua Mei 18.

Lampard alisema suala la watu kukaa mbalimbali limefanikiwa nchini humo lakini ana hofu kama jambo hilo linaweza kufanyika kwa kiwango hicho katika soka.

“Tutaweza vipi kudhibiti wachezaji kutogusana wakati wa mazoezi kwa wiki chache ambazo watakuwa wakijifua, je kama kutajitokeza changamoto nini kifanyike? alihoji Lampard.

Sergio ‘Kun’ Aguero wa Manchester City alipaza sauti akidai ana hofu baada ya kurejea katika mazoezi wanaweza kuziambukiza familia zao kwa kuwa itawalazimu kugusana.

Kwa mujibu wa maelekezo, timu zitacheza nje ya viwanja vyao kuepuka mikusanyiko ya watu ingawa orodha iliyopendekezwa ni watu wasiozidi 300.

Lampard alisema kitendo cha kucheza ugenini kinahitaji uadilifu wa aina yake kwa timu zote mbili zinapocheza.

“Kuna suala la uadilifu ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini timu zinapocheza viwanja vya ugenini,”alisema kocha huyo.

Klabu zimekubaliana kutumia viwanja vinane kwa mashindano endapo serikali itakubali ligi kurejea.

Wakati vigogo wa Chama cha Soka England (FA) wakijadili namna bora ya kurejesha ligi hiyo, suala la mikataba ya wachezaji linawaumia vichwa.

Wadau wa soka akiwemo Lampard ana hofu kama suala hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi kutokana na mkanganyiko uliojitokeza.

Idadi kubwa ya wachezaji mikataba yao inamalizika Juni 30 wakati ligi mbalimbali ndio zinatarajiwa kurejea.

“Kuna wachezaji wengi watakuwa nje ya mikataba, hili ni jambo kubwa ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini,”alisema Lampard.

Chelsea ina majina makubwa ya wachezaji watatu ambao watakuwa nje ya mkataba Willian, Pedro na Olivier Giroud hatua ambayo inampa hofu kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo na timu ya taifa ya England.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...