
Madrid, Hispnia. Barcelona inajiandaa kuwauza wachezaji wanane wa kikosi cha kwaza wakiwemo Antoine Griezmann, Ousmane Dembele na Luis Suarez.
Klabu hiyo inataka kuboresha kikosi chake katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao na mastaa hao wanatarajiwa kuwekwa sokoni.
Barcelona inataka kuwauza wachezaji hao ili kupata fedha za kununua wapya wenye viwango bora vya ushindani.
Miongoni mwa majina makubwa yanayotajwa kuuzwa ni Griezmann ambaye alitua Barcelona akitokea Atletico Madrid majira ya kiangazi msimu uliopita kwa Pauni89 milioni.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa inadaiwa haivi chungu kimoja na nahodha wake Lionel Messi tangu alipojiunga na klabu hiyo.
Messi alitoa mapendekezo ya kusajiliwa Neymar akitoka PSG kwenda kuunda tena safu imara ya ushambuliaji.
Griezmann amefunga mabao 14 katika mechi 37 za Barcelona wakati Dembele amekuwa na majeraha ya mara kwa mara yanayomuweka nje.
Mastaa wengine wanaotarajiwa kuuzwa ni Arturo Vidal, Ivan Rakitic, Samuel Umtiti, Nelson Semedo na Sergi Roberto ambao Barcelona yenye maskani Nou Camp inataka kuwapunguza.
No comments:
Post a Comment