Search This Blog

Sunday, May 17, 2020

Mambo magumu kwa Said Ndemla ndani ya SIMBA



SAID Ndemla nyota wa Klabu ya Simba msimu huu 2019/20 mambo yamekuwa magumu kwake kutokana na kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza.

Simba ikiwa imecheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 amecheza mechi tatu pekee ambazo ni dakika 270.

Ndemla amekosekana kwenye mechi 25 ambazo ni dakika 2,250 ndani ya Uwanja akijenga ushkaji na benchi.

Chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems amecheza mechi mbili ambapo ilikuwa mbele ya Biashara United na Singida United, huku chini ya Sven Vandenbroeck akionekana kwenye mechi moja dhidi ya Ndanda FC.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 71 kibindoni na imetupia mabao 63.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...