Search This Blog

Sunday, May 17, 2020

Machafuko yaendelea kuongezeka katika mkoa wa Ituri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Machafuko yanaripotiwa kuongezeka katika mkoa wa Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuzidi kuzusha wasiwasi miongoni mwa raia wa mkoa huo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, mashambulio kadhaa yameripotiwa katika maeneo 4 kati ya 5 ya mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo.

Wiki hii, Wabunge na Maseneta kutoka mkoa wa Ituri walikutana na Jeanine Mabunda na Alexis Thambwe Mwamba, Maspika wa Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti, ili kuomba hatua zaidi kutoka kwa mamlaka zichukuliwe dhidi ya makundi yanayohusika na machafuko hayo katika maeneo hayo.

Mwezi uliopita Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) ilisema katika ripoti yake kuwa, zaidi ya watu 150 wameuawa katika mkoa wa Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha siku 40 zilizopita.


Mamia ya Wakongomani wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo wa ADF-Nalu  ambao asili yao ni Uganda hususan katika maeneo ya mashariki mwa nchi, tokeo mwaka 2014.

Wiki iliyopita, wanamgambo 23 waliuawa katika mapigano baina yao na Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) katika mkoa wa Ituri, kaskazini mwa nchi.

Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likishuhudia machafuko ya mara kwa mara baina ya makundi ya wanamgambo kwa upande mmoja na wanamgambo na maafisa usalama kwa upande mwingine, kutokana na kuwa na utajiri mkubwa wa madini hususan dhahabu na almasi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...