Search This Blog
Sunday, May 3, 2020
Hispania: Watu waruhusiwa kutembea nje kwa mara ya kwanza
Wakati huo huo baadhi ya mataifa ya Ulaya kwa tahadhari yalilegeza vizuwizi vya kutoka nje, wakati Urusi na Ujerumani zimeripoti ongezeko la maambukizi.
Wakati serikali zikitafakari kuondoa vizuwizi vya kuwataka wananchi kubakia majumbani ili kuanzisha tena uchumi wao, maafisa nchini Marekani wameleta matumaini kiasi kwa kuidhinisha dawa ya majaribio ili itumike kwa wagonjwa wa ugonjwa wa COVID-19
Uamuzi huo ulikuwa wa hivi karibuni kabisa katika hatua za dunia kutafuta dawa na chanjo kwa ajili ya virusi vya corona, ambavyo vimesababisha nusu ya binadamu dunia kuwamo katika vizuwizi vya kutoka nje na kuuweka uchumi wa dunia kuelekea katika mporomoka mbaya kabisa tangu mdororo mkuu katika miaka ya 1930.
Virusi sasa vimewauwa zaidi ya watu 242,000 duniani kote, kwa mujibu wa idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la AFP, na walioambukizwa wanafikia milioni 3.4 tangu kuzuka mara ya kwanza virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka jana.
Kukiwa na ishara kwamba janga hili linapungua kasi katika mataifa yale yaliyoathirika zaidi , mataifa ya Ulaya pamoja na baadhi ya sehemu za Marekani yameanza kuondoa vizuwizi kujaribu kurejesha hali ya maisha kuwa ya kawaida katika uchumi ambao ulioathirika kutokana na wiki kadhaa za kufungwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment