Mwimbaji huyo amesema Mavoko ni miongoni mwa wasanii waliomvutia sana hadi kuingia kwenye muziki wa Bongo Fleva na kama ikitokea nafasi kwenye lebo yake atafanya hivyo.
“Ikitokea nafasi haiwezi kushindikana, Rich ni Kaka yangu ameni-inspire,” Harmonize ameiambia XXL ya Clouds FM Jumanne hii.
Katika hatua nyingine amefunguka kuhusu ujumbe alioandika mtandaoni hivi karibuni kuhusu Rich Mavoko akihoji kwanini kuna baadhi ya watu wanafurahia ukimya wake na kueneza maneno ambayo sio sahihi.

No comments:
Post a Comment