Search This Blog
Thursday, May 7, 2020
Faiza awapiga bao mastaa
MFANYABIASHARA maarufu kwa sasa kwa upande wa wasanii Bongo Muvi, Faiza Ally, ambaye pia ni ‘baby mama’ wa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amewafunga midomo mastaa wa Bongo Muvi kwa kuporomosha mjengo wa hatari.
Akizungumza , Faiza alisema kuwa hakuna kitu kizuri kama jitihada kwenye maisha ya kila siku.
“Nyumba ambayo mnaiona kwenye mitandao niliwahi kuiposti wanangu wapo hapo iko Dodoma, ni yangu na niliijenga kwa nguvu zangu unazoziona nahangaika kila kukicha, lakini nimenunua kiwanja kandokando ya bahari kabisa huko Kigamboni,” alisema Faiza.
Mwanamama huyo ambaye ni kama ameipa kisogo sanaa, alisema ameona hakuna njia zaidi ya kuchakarika na kutafuta maisha kwani mambo yanaenda tofauti sana kwa hivi sasa, hivyo anatengeneza maisha kwa ajili ya wanawe.
“Sijui nisemaje, jamani hakuna kitu kizuri kama jitihada maishani, nilikuwa natamani hivi ambavyo ninavyo hivi sasa na kweli Mungu amenipa na anaendelea kunipa lakini ningejibweteka sidhani kama ningepata hivi vyote,” alisema Faiza ambaye anaonekana wazi kuwaacha mbali kabisa mastaa mbalimbali wa Bongo Muvi kwa jitihada anazozifanya.
Mastaa wengi Bongo Muvi hususan wa kike hawana zaidi huishi nyumba za kupanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment