Search This Blog
Thursday, May 7, 2020
Ethiopian Airlines: Tuko tayari kusaidia mashirika ya ndege yaliyokwamishwa na corona
Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) linajiandaa kuyaokoa mashirika ya ndege yaliyokwama katika ubebaji mizigo licha ya kwamba shirika hilo nalo lina matatizo mengi hivi sasa kutokana na hasara linazopata baada ya ndege zake kusimamisha safari kwa sababu ya corona.
Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Tewolde GebreMariam amesema kuwa, sasa hivi mazungumzo yanaendelea kati ya shirika hilo na serikali ya Mauritius kutokana na ndege za nchi hiyo kukwama katika ubebaji mizigo. Hata hivyo amesema, ingawa hivi sasa mazungumzo kati ya shirika hilo na Afrika Kusini hayajaanza rasmi lakini hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa ili kuisaidia nchi hiyo katika mgogoro wa kukwama mizigo yake.
Aidha amesema, sasa hivi serikali ya Mauritius inafikiria kufunga mkataba wa kubeba mizigo na shirika la Ethiopian Airlines na mazungumzo yanaendelea kuhusu ufanikishaji wa jambo hilo.
Hivi sasa Shirika la Ndege la Afrika Kusini limefilisika katikati ya vita vya kupambana na corona. Shirika la ndege la Kenya Airways nalo limeomba msaada likijipanga zaidi kusubiri lini litaanza upya safari zake.
Mashirika makubwa ya ndege duniani yameingia kwenye mgogoro mkubwa ambao haujawahi kuyatokea baada ya kuzuka wimbi la maambukizo ya kirusi cha corona. Mashirika mengi makubwa yameomba misaada kutokana na safari zao takriban zote kusimamishwa kwa sababu ya COVID-19. Shirika la Ethiopian Airlines limetangaza kupata hasara ya takriban dola bilioni moja za mauzo ya tiketi katika mwaka wake wa fedha unaomalizika mwezi ujao wa Juni.
Mapema mwezi Januari mwaka huu, shirika la Ethiopian Airlines lilikuwa na mazungumzo na Afrika Kusini na linapenda kuwa sehemu ya mashirika yenye mikataba na Afrika Kusini. Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Tewolde GebreMariam amesema: "Tunadhani tunaweza kuwakabili na kuanza mazungumzo nao katika mazingira mapya."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment