Search This Blog
Sunday, May 10, 2020
CHINA: Marekani haitofika popote kwa kutumia vibaya azimio nambari 2231
Chen Xu, Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mapatano ya JCPOA ni mapatano ya pande kadhaa na kusisitiza kuwa, juhudi za kutumia vibaya azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hazitofikia popote.
Mwakilishi huyo wa China katika Umoja wa Mataifa ameyasema hayo kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kubainisha kwamba mapatano ya JCPOA yalikuwa ya pande kadhaa ambayo yalipata uungaji mkono wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwa mtazamo wa kisheria ni lazima yatekelezwe. Aidha Xu amezitaka pande zote husika za mapatano hayo kutekeleza ahadi zao ndani ya JCPOA. Sambamba na kukaribia muda wa kufutwa vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambavyo pia ni sehemu ya azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la UN, Wamarekani wanafanya njama kubwa kujaribu kuzuia kuhitimishwa vikwazo hivyo.
Hivi karibunii, serikali ya Marekani ilisambaza utangulizi wa azimio kwa wanachama wa baraza hilo ikiwataka warefushe muda wa vikwazo vya silaha vya umoja huo dhidi ya Iran. Pamoja na hayo upitishwaji wa azimio hilo unategemea kuungwa mkono na wanachama 9 wa Baraza la Usalama tena bila kupigiwa kura ya veto na China na Russia. Pamoja na kwamba Marekani kwa miaka miwili iliyopita na bila kuzingatia azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama, ilijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, inadai katika tafsiri yake mpya kwamba kwa mujibu wa azimio hilo bado ni mmoja wa wanachama wenye taathira katika JCPOA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment