MBUNGE wa Nanyamba(CCM), Abdallah Chikota ameiomba serikali kusimamia upatikanaji wa magunia kwa wakati ili kuzuia ubora wa korosho kutoathirika.
Sambamba na hilo, ameiomba Wizara ya Kilimo kuhakikisha suala la upatikanaji wa vifungashio haliachiwi kwa Bodi ya Korosho peke yake bali lihusishe hata vyama vya ushirika ili kupunguza kabisa upungufu wa magunia katika msimu.
Akichangia leo Bajeti ya Wizara ya Kilimo bungeni jijini Dodoma, Chikota amesema vifungashio vikipatikana kwa wakati itasaidia kuhifadhi ubora wa korosho.
“Naiomba wizara isimamie ipasavyo magunia yapatikane kwa wakati ili korosho zetu zisije kuathirika ubora wake,lakini niiombe wizara pia siachie suala hili bodi ya korosho peke yake bali vyama vya ushirika vihusike pia,”ameomba Chikota.
Ameshauri pia pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea ya sulphur zipatikane kwa wakati ili isiathiri msimu wa kilimo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment